KITUO CHA HUDUMA NA SHERIA YAZINDUA
VITABU VIWILI (2) VYA
SHERIA
Kituo cha Huduma na Sheria
Zanzibar (ZLSC) leo tarehe 10/10/2011 kimeadhimisha siku ya Adhabu ya
kifo
na kuzindua vitabu
viwili (2) vya
Sheria.
Mgeni rasmi katika kuadhimisha
siku ya Adhabu ya kifo na uzinduzi wa vitabu hivyo alikuwa
Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi.
Ujumbe (theme) wa mwaka huu wa kuadhimisha siku ya
Adhabu ya kifo ulikuwa unyama wa Adhabu ya kifo
(The humanity of Death
Penalty).
Vitabu viwili vilivyozinduliwa
ni Adhabu ya Kifo katika Sheria za Kiislamu
(Death Penalty in Islamic Law) kilichotungwa na Dk. Muhyiddin Ahmad Khamis (Maalim
Siasa).
Kitabu cha pili ni
Zanzibar; The Development of the
Constitution, kilichohaririwa na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya ZLSC, Profesa Chris Maina
Peter na Wakili
wa Canada Immi Sikand.
Uzinduzi wa
vitabu
hivi viwili
kumeongeza idadi ya vitabu vilivyochapishwa na
ZLSC kuwa ni kumi na sita
(16).
Maudhui ya kitabu cha Adhabu ya
Kifo katika Sheria za Kiislamu ni Adhabu ya Kifo katika nidhamu
ya Uislamu ni nyenzo katika nyenzo ambazo zinategemewa katika
kuhifadhi jamii kuepukana na kukengeuka na uovu na kwa ajili ya
kutia adabu mkosaji.
Aidha, maudhui ya kitabu
cha,
Zanzibar; The Development of the
Constitution kinachoelezea historia ya
maendeleo ya Katiba Zanzibar na marekebisho ya kumi
ya 2010 Katiba ya Zanzibar yaliyopelekea
kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) Zanzibar
|